Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Mhe.
Edward Rutakangwa kuwa kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama katika
hafla fupi iliyofanyika leo Ikulu jijini Dares salaam
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Mh. Semistocles Kaijage (kulia) kuwa
jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kabla ya
uteuzi huo Mh. Semistocles Kaijage alikuwa jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu
kanda ya Dar es salaam.
ais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akifuarahia
Jambo na kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. Edward Rutakangwa
(wa tatu kutoka kulia) mara baada ya kumwapisha leo Ikulu jijini Dar
es Salaam. Wengine kutoka kulia ni Jaji wa mahakama ya Rufani Mussa
Kipenka na Jaji Semistocles Kaijage (wa kwanza kushoto).
Mh.
Rufani Mussa Kipenka akipongezwa na baadhi ya ndugu waliohudhuria
hafla fupi ya kuapishwa kwake kuwa jaji wa mahakama ya Rufani Ikulu
jijini Dar es salaam.
Jaji wa mahakama ya Rufaa Mh. Semistocles Kaijage akizungumza na
vyombo vya habari mara baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es
salaam. Pamoja na mambo mengine amesema atahakikisha kuwaanatekeleza
majukumu yake kwa kuzingatia sheria,kupunguza mlundikano wa kesi na
kuhakikisha kuwa maamuzi yanatolewa kwa haki.
Jaji wamahakama ya Rufani Mh. Mussa Kipenka akisaini hati ya
kiapo mara baada ya kuapishwa na Rais Dkt. Jakaya kikwete leo Ikulu
jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni jaji mkuu wa Tanzania Mohammed
Chande Othman.
No comments:
Post a Comment