Saturday, June 9, 2012

TSN yajitetea Sakata la Athumani Hamisi



Tarehe 5 Juni,2012, mfanyakazi waKampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), ambaye amelemaa baada ya kupata ajali yagari, Bwana Athumani Hamisi, aliitisha mkutano wa waandishi wa habari kwenyeukumbi wa Maelezo, Dar es Salaam, na kutoa taarifa iliyojenga taswira kuwaametelekezwa na TSN pamoja na Serikali.

TSN inapenda kufafanua kuwa Serikalina kampuni hii, ambayo ilimwajiri Athumani tarehe 1/09/2006 kama Mpiga pichaMwandamizi, wamemhudumia mfanyakazi huyo kikamilifu tangu alipopata ajalitarehe 12 Septemba, 2008 hadi sasa, na huduma hiyo inaendelea.

Baada ya kutokea ajali hiyo, TSN kama mwajiri ilisimamia matibabu yake ya awali katikahospitali ya Taifa ya Muhimbili Kitengo cha Mifupa (MOI) mpaka Serikali, kwakupitia Wizara ya Afya ilipomhamishia  Netcare Rehabilitation Hospital nchini AfrikaKusini kwa matibabu zaidi.
 
Serikali ililipia gharama za matibabuyake yote akiwa Afrika Kusini kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi saba, ambayoyanazidi shilingi milioni mia moja.Gharama hizo ni pamoja na ununuzi wa kigari maalum ambacho Athumani anatumiasasa.

TSN kama mwajiri ililipa nauli yandege kwenda na kurudi pamoja na posho ya kujikimu ya mgonjwa pamoja na nduguwasindikizaji ambao ni Bw. Hassan Hussein na  Bi. Mirriam Malaquias.Posho yakujikimu ilikuwa USD 6,210 sawa na Shilingi 9,315,000, na  nauli kwa watu watatu ilikuwa ni Shilingi3,535,869.92. Athumani aliendelea kupatiwa huduma akiwa huko Afrika Kusini kwagharama za Serikali na TSN mpaka aliporejea nchini tarehe 08/05/2010. Gharamazilizolipwa na kampuni kwa mfanyakazi huyu hadi sasa ni takriban shilingi million 52.

Athumani aliporejea nchini alilakiwana wafanyakazi na viongozi wa TSN na kupangiwa chumba hoteli ya Holiday Inn wakatiutaratibu wa kumtafutia nyumba ya kupanga ukikamilishwa. Kampuni ilitumia kiasicha Shilingi 1,756,979.50 kulipia hoteli. Baadaye alipelekwa kwenye nyumbaambayo alipangiwa na Kampuni katika eneo la Sinza Vatican ambapo ndipo badoanaishi hadi hivi sasa. Gharama ya nyumba kwa mwaka wa kwanza 2010 ilikuwa niShilingi 4,200,000 au Shilingi 350,000 kwa mwezi.  Mwaka 201 mwenye nyumba alipandisha kodi hadi400,000 kwa mwezi ambapo Kampuni ililipia Shilingi 4,800,000. Kodi hiyoimeishia Mei mwaka huu na kampuni imeshafanya mazungumzo na mwenye nyumba iliAthumani aendelee kuishi hapo kwa muda wakati mipango endelevu ya ustawi wakeinafanywa kwa kuzingatia taratibu za ajira.

Mnamo tarehe 8/12/2010 Athumanialirudi tena Afrika Kusini kwa ajili ya uchunguzi wa maendeleo ya afya yake namatibabu yaligharimiwa na Serikali wakati TSN iligharamia nauli yake na yamuuguzi wake, pamoja na posho ya kujikimu Shilingi 6,300,000/-.

Pamoja na bwana Athumumai kulalakitandani kwa muda wote huo ameendelea kulipwa mshahara kamili bila kukatwakama mfanyakazi wa kawaida ikiwa ni msaada wa kampuni kwa kuzingatia ulemavualioupata.Mshahara aliolipwa kwa muda wote aliokuwa anaugua ni kiasi chashilingi 26,773,000. Vile vile kampuni ilimlipa muuguzi toka Afrika Kusiniambaye alikuwa anamhudumiaa Athumani  Rand 12,500 kama mshahara wake.

Kuanzia Januari 2011, mshahara waAthumani umejumuisha asilimia 15 kama posho ya nyumba ambayo wafanyakazi wotewanalipwa. Aidha  Athumani yupo kwenyempango wa bima ya afya anayolipiwa na kampuni, ambayo inamwezesha yeye nafamilia yake kuweza kutibiwa katika hospitali yoyote hapa Tanzania.  Kampuni inamlipia Shilingi 68,449.20 kilamwezi na bima hiyo ndiyo inayogharamia matibabu yake yote hapa nchini.
 
Bwana Athumani anapatiwa usafiri naTSN mara mbili kwa wiki kumtoa nyumbani hadi Muhimbili na kurudi kwa ajili yamazoezi ya viungo. 
Imetolewa na
OFISI YAMHARIRI MTENDAJI
08.6.2012

No comments:

Post a Comment