Habari kutoka Somalia zinaarifu kuwa, watu wenye silaha wasiojulikana wamemuua kwa kumfyatulia risasi mwandishi mmoja wa habari nchini humo.
Habari zaidi kutoka Mogadishu, leo zimemnukuu mmoja wa makamanda wa jeshi la Somalia Dhahir Aden kuwa, mwandishi huyo wa habari aliyekuwa akifanya kazi katika televisheni ya taifa, aliuawa usiku uliopita na kwamba hadi sasa bado polisi wanaendelea na uchunguzi kamili wa tukio hilo.
Aden amemtaja mwandishi huyo kuwa, ni Ahmed Farah Ilyas na kwamba, hadi sasa hakuna mtu aliyetiwa mbaroni kufuatia tukio hilo. Huyo ni mwandishi wa habari wa 16 kuuawa tangu mwanzoni mwa mwaka huu katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
No comments:
Post a Comment