Meneja
wa Shirika la Posta mkoani Mwanza, Julius Chifungo, akizunguza kwenye
Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani ambayo kimkoa yamefanyika leo
katika Shule ya Saint Mary's Seminary (Nyegezi Sekondari) Jijini Mwanza.
SIKU
ya Posta duniani huadhimishwa ifikapo Oktoba 09 kila Mwaka ikiwa ni
sehemu ya kumbukumbu ya Siku ya kuanzishwa kwa Umoja wa Posta Duniani
ulioanzishwa mwaka 1874 katika mji wa Berne nchini Switzerland
ukijumuisha mataifa 192 duniani.
Na BMG
Maadhimisho
hayo yamekwenda sambamba na zoezi la kukabidhi zawadi kwa Washindi wa
Uandishi wa barua Kitaifa kutoka mkoani Mwanza ambapo washindi watano
kati ya 10 bora kitaifa wametoka Saint Mary's Seminary (Nyegezi
Sekondari) Jijini Mwanza.
Washindi
hao na nambari walizoshika kwenye mabano ni, Denis Bahati Stephen (01),
Samwel Lufungulo Somelo (02), Vitalis Aloo Awasi (03), Kizito Eliakimu
Paschal (04) na Fredrick Elias Mayunga (08).
Washindi
wa Tano na Sita wametoka Shule ya Mazinde Juu mkoani Tanga, Mshindi wa
Saba ametoka Shule ya Lugalo mkoani Iringa, huku Washindi wa Tisa na 10
pia wakitoka Shule ya Mazinde Juu mkoani Tanga.
Meneja
wa Posta mkoani Mwanza, Julius Chifungo amesema shindano la uandishi wa
barua huwashirikisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari
wasiozidi umri wa miaka 15 ambapo shule za msingi lugha ya kiswahili na
kiingereza hutumika na kiingereza pekee kwa shule za sekondari.
Amebainisha
kwamba wanafunzi huandika barua yenye mane kati ya 500 na 1,000
kulingana na mada iliyotolewa na kwamba mwaka huu mada ilikuwa ni
"Jiandikie barua ukiwa na miaka 45" ambapo barua ya mshindi wa kwanza
itakwenda kushindanishwa na barua za washindi wengine kutoka nchi 191
wanachama wa Umoja wa Posta Duniani ambapo mshindi wa kwanza nchini
ataliwakilisha taifa kwenye shindalo hilo nchini Switzerland.
Katibu
Mtendaji wa Idara ya Elimu, Jimbo Kuu la Mwanza, Alex Masasi, ambaye
alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo akizungumza ambapo
amewahimiza wanafunzi kuongeza bidii katika masomo yao hususani kuwa
bora kwenye kusoma, kuandika na kuzungumza lugha nyingi tofauti na
kiswahili na kiingereza.
Wanafunzi
wakimsikiliza kwa umakini Katibu Mtendaji wa Idara ya Elimu, Jimbo Kuu
la Mwanza, Alex Masasi, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho
Siku ya Posta yaliyofanyika leo Jijini Mwanza.
Mkuu
wa Shule ya Saint Mary's (Nyegezi Sekondari) Jijini Mwanza, akizungumza
kwenye Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani. Siku ya Posta duniani
hufanyika kila mwaka Oktoba 08, hivyo yamefanyika leo Oktoba 07 kutokana
na ratiba ilivyopangwa.
Mshindi
wa Nane Kitaifa kwenye Mashindano ya Uandishi wa barua, Fredrick Elias
Mayunga kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akipokea zawadi yake.
Mshindi
wa Nane amepokea Cheti cha utambuzi, Tisheti, Kamusi ya Kiingereza,
begi la kubebea daftari, Kikokoteo pamoja na fedha Elfu Arobaini
(40,000).
Mshindi
wa Nne Kitaifa kwenye Mashindano ya Uandishi wa barua, Kizito Eliakimu
Paschal, kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akipokea zawadi
yake.
Mshindi
wa Nne amepokea Cheti cha utambuzi, Tisheti, Kamusi ya Kiingereza, begi
la kubebea daftari, Kikokoteo pamoja na fedha Laki Moja na Elfu
Ishirini (120,000).
Mshindi
wa tatu Kitaifa kwenye Mashindano ya Uandishi wa barua, Vitalis Aloo
Awasi, kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akipokea zawadi yake.
Mshindi
wa Tatu amepokea Cheti cha utambuzi, Tisheti, Kamusi ya Kiingereza,
begi la kubebea daftari, Kikokoteo pamoja na fedha Laki Mbili (200,000).
Mshindi
wa Pili Kitaifa kwenye Mashindano ya Uandishi wa barua, Samweli
Lufungulo Somelo, kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akipokea
zawadi yake.
Mshindi
wa Pili amepokea Cheti cha utambuzi, Tisheti, Kamusi ya Kiingereza,
begi la kubebea daftari, Kikokoteo pamoja na fedha Laki Tatu (300,000).
Mshindi
wa Kwanza Kitaifa kwenye Mashindano ya Uandishi wa barua, Denis Bahati
Stephen, kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akipokea zawadi
yake.
Mshindi
wa kwanza amepokea Cheti cha utambuzi, Tisheti, Kamusi ya Kiingereza,
begi la kubebea daftari, Kikokoteo pamoja na fedha Laki Nne (400,000).
Mkuu
wa Shule ya Saint Mary's Seminary, Maximillian Buluma, akipokea zawadi
ya shule hiyo baada ya kuwa shule iliyotoa washindi kitaifa pamoja na
washiriki wengi. Amepokea mpira pamoja na Cheti kutoka Shirika la Posta.
Kulia ni Meneja wa Posta Mwanza, Julius Chifungo, akimkabidhi mgeni rasmi zawadi.
Washindi
wa shindano la kuandika barua nchini, wakiwa katika picha ya pamoja na
viongozi wa Shirika la Posta Mwanza, Waalimu wa Saint Mary's Seminary
Jijini Mwanza, Mgeni Rasmi pamoja na Wazazi.
Washindi
wa shindano la kuandika barua nchini kutoka shule ya Saint Mary's
Seminary Jijini Mwanza wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wazazi wao.
Washindi wa shindano la kuandika barua nchini, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Posta Mwanza.
Washindi
wa shindano la kuandika barua nchini, wakiwa katika picha ya pamoja na
Mkuu wa shule ya Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza, Mgeni Rasmi pamoja
na Meneja wa Posta Mwanza.
Washindi wa shindano la kuandika barua nchini kutoka shule ya Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza.
Washindi wa tatu bora katika shindano la kuandika barua nchini kutoka shule ya Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza.
Afisa Masoko, Shirika la Posta mkoani Mwanza, Julius Mponda, akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mwalimu
Victor Mgisha anayefundisha somo la Kiingereza shule ya Saint Mary's
Seminary Jijini Mwanza akizungumza kwenye Maadhimisho hayo.
Waalimu
wa Shule ya Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza wakielezea furaha yao
baada ya wanafunzi wa shule hiyo kuibuka washindi wa shindano la
uandishi wa barua linaloandaliwa na Umoja wa Posta duniani na kufanyika
kwa nchi wanachama 191 kote duniani.
Mwalimu
wa Shule ya Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza, akisoma barua iliyompa
ushindi, mshindi wa kwanza kwenye shindano la uandishi wa barua nchini.
Meneja
wa Shirika la Posta mkoani Mwanza, Julius Chifungo, akizunguza kwenye
Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani ambayo kimkoa yamefanyika leo
katika Shule ya Saint Mary's Seminary (Nyegezi Sekondari) Jijini Mwanza.
Mshindi
wa kwanza Kitaifa kwenye shindano ya uandishi wa barua, Denis Bahati
Stephen, kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akizunguza
kwenye Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani ambayo kimkoa yamefanyika
leo katika Shule ya Saint Mary's Seminary (Nyegezi Sekondari) Jijini
Mwanza.
Mshindi wa pili Kitaifa katika shindano ya uandishi wa barua, Samweli Lufungulo Somelo, kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akizunguza
kwenye Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani ambayo kimkoa yamefanyika
leo katika Shule ya Saint Mary's Seminary (Nyegezi Sekondari) Jijini
Mwanza.
Bonyeza HAPA Kutazama Mwanza walivyoibuka kidedea kwenye Shindano la Uandishi wa barua mwaka 2015 Kitaifa.
No comments:
Post a Comment