Filamu kadhaa za Iran zitaonyeshwa katika Awamu ya Saba ya Tamasha ya Kimataifa ya Filamu ya Kenya itakayoanza tarehe 24 Oktoba hadi 3 Novemba mwaka huu wa 2012.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Nairobi, filamu za Iran zitakazoonyeshwa katika tamasha hiyo ni zile zilizoonyeshwa katika Tamasha ya Filamu ya Moqawama Iran mwaka 2012.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa katika usiku wa tarehe 27 Oktoba kuanzia saa kumi na mbili jioni kutakuwa na maonyesho maalumu ya filamu za Iran katika Ukumbi wa Louis Leakey katika Jengo la Makumbusho la Kenya (National Museums of Kenya).
Sekta ya filamu nchini Iran imestawi kwa kiwango kikubwa na kiasi kwamba filamu moja ya Iran ilipata zawadi katika Tamasha ya Oscar nchini Marekani. Watazamaji filamu duniani huvutiwa na filamu za Iran kwa sabau zinazingatia maadili bora mbali na kutoa mafunzo mbalimbali kwa watu wa matabaka yote ya jamii.
No comments:
Post a Comment