Marekani na Umoja wa Ulaya zimeleezea wasiwasi wao kuhusu hali ya kisiasa nchini Lebanon, ambako upinzani umemtaka waziri mkuu ajiuzulu kuhusiana na mlipuko mkubwa uliotokea nchini humo wiki iliyopita na kuinyooshea kidole cha lawama Syria.
Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton ameonya dhidi ya pengo la kisiasa nchini Lebanon, wakati akikamilisha ziara yake nchini humo, akiunga mkono maoni kutoka Wizara ya Mambo ya kigeni ya Marekani.
Bibi Ashton pia alionya kuwa kuna baadhi ya watu wanaojaribu kuyageuza mawazo kutoka kwa hali halisi katika eneo hilo kwa kusababisha matatizo nchini Lebanon.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya kigeni ya Marekani Victoria Nuland alisema Marekani inaunga mkono juhudi za Rais Michel Sleiman na viongozi wengine kuunda serikali madhubuti.
No comments:
Post a Comment