Ujerumani leo imezindua kumbusho la kitaifa la mamia kwa maelfu ya Waroma na Wasinti waliouwawa wakati wa utawala wa Wanazi, huku Kansela Angela Merkel akisema kila kifo kilichotokea kinamsababishia maombolezo na aibu
Kumbusho hilo lililokuwa likisubiriwa tangu zamani limejengwa mfano wa hodhi lenye maji na mnara ambao juu yake ua litakuwa likiwekwa kila siku.
Kumbusho hilo linakutikana karibu na jengo la bunge katikati ya mji mkuu Berlin, na pia karibu na makumbusho mengine mawili ya wahanga wa ukatili wa wanazi: moja likiwa la wayahudi milioni sita na jengine dogo la mashoga.
Wanahistoria wanakadiria kuwa kati ya Wasinti na Waroma 220,000 na 500,000 barani Ulaya waliuawa na wanazi, waliowachukulia kuwa tabaka la walio wachache.
Kansela Merkel aliungana na mamia ya manusura wa mauaji hayo ya halaiki wakiongozwa na kiongozi wa Baraza kuu la Wasinti na Waroma nchini Ujerumani, Romani Rose pamoja na rais Joachim Gauck.
No comments:
Post a Comment