Baraza la umoja wa mataifa limefungua rasmi mkutano wake mjini New York.
Rais Barack Obama amefungua mkutano huo kwa
hotuba ya kumsifu balozi wa zamani wa Libya ambaye aliuawa katika
shambulizi dhidi ya ubalozi wa Marekani mjini Benghazi mapema mwezi huu.Alilaani ghasia hizo zilizotokea kufuatia ghadhabu katika nchi za kiisilamu baada ya kutolewa kwa filamu iliyokejeli Mtume Muhammad na dini ya kiisilamu.
Obama amelaani filamu hiyo na kusema Marekani haina uhusiano wowote na filamu hiyo na vile vile amelaani waliotengeza filamu hiyo.
Rais Obama ameitaka serikali ya rais wa Syria Bashar Assad kuondoka mamlakani na kuwa Marekani itafanya kila iwezalo kuzuia Iran kuwa na zana za nuklia.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, naye katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon, alikitaja kipindi hiki kama kipindi cha msukosuko ,mpito na mageuzi.
Alionya kuwa fursa inaweza kuwa inatoweka ya kupata suluhu baina ya Israil na Wapalestina, ya kuwa na mataifa mawili.
No comments:
Post a Comment