Wednesday, September 26, 2012

Ban: Vita nchini Syria ni maafa yanayotishia amani ya dunia

Katibu  mkuu  wa  umoja  wa  mataifa  Ban Ki-moon amesema  leo  kuwa  vita vya  ndani  nchini  Syria  ni maafa  ambayo  sasa  yanatishia  amani  ya  dunia  na ametaka  ichukuliwe  hatua   na  baraza  la  usalama  la umoja  wa  mataifa  ambalo  limegawanyika

. Ban amesema katika  hotuba  yake  ya  ufunguzi  wa  baraza  kuu  la umoja  wa  mataifa  kuwa  mzozo  wa  Syria  unageuka kuwa  maafa  ya  eneo  hilo ukiwa  na  athari  duniani, ambazo  zinahitaji  kuchukuliwa  hatua  na  baraza  la usalama.


 Ban amewaambia  viongozi  wa  dunia  kuwa jumuiya  ya  kimataifa  haipaswi  kuangalia  kando  wakati ghasia  zinazidi  kuongezeka  na  kufikia  hatua  ya kutoweza  kudhibitiwa  tena, na  ameongeza  kuwa  ukiukaji wa  kinyama   wa  haki  za  binadamu  unafanywa  na majeshi  ya  serikali  ya  rais Bashar al-Assad. Katibu  mkuu  Ban  ameongeza  kuwa , jumuiya  ya kimataifa  inapaswa  kuzuwia  ghasia  hizo  na  kuzuwia kuingizwa  kwa  silaha  kwa  pande  zote  na  kuanzisha serikali  itakayoongozwa  na  uongozi  wa  mpito  haraka iwezekanavyo.

Ameitaka  jumuiya  ya  kimataifa , hususan wanachama  wa  baraza  la  usalama  la  umoja  wa mataifa  na  nchi  za  eneo  la  mashariki  ya  kati  kuunga mkono  kwa  dhati  juhudi  za  mjumbe  wa  umoja  wa mataifa  na  umoja  wa  nchi  za  Kiarabu  Lakhdar Brahimi.

No comments:

Post a Comment