Wednesday, September 26, 2012

Obama ahutubaia hadhara kuu ya Umoja mataifa

Rais Barack Obama wa Marekani amelihutubia Baraza kuu la Umoja wa mataifa  na kusema kwamba  tawala zinazokandamiza  jamii zao hazina nafasi katika  Umoja  wa mataifa. Akigusia kuhusu Syria alisema wakati umefika kwa rais Bashar al-Assad  aondoke madarakani na akapongeza mageuzi yaliopatikana nchini Misri, Libya na Yemen, akisema Marekani daima itasimama upande wa wanaopigania haki.

 Kiongozi huyo paia aligusia juu ya  kustawi kwa demokrasia  barani Afrika, akitaja juu ya uchaguzi wa Rais hivi karibuni  nchini Malawi, Senegal na Somalia. Akigusia juu ya wimbi la maandamano kupinga filamu iliyoukashifu Uislamu na Mtume Mohammad, Obama alisema filamu hiyo imewakasirisha pia wamarekani  na kukumbusha kuwa  kuna Wamarekani walio Waislamu.


Lakini pamoja na hayo alisema katiba ya nchi yake inasisitiza juu ya uhuru wa kutowa maoni. Aliuchekesha ukumbi wa mkutano aliposema yeye binafsi kila siku anakashifiwa. Rais Obama pai alizungumzia  mzozo kati ya  Israel na  Palestina na kutilia mkazo tena juu ya  ugumu lakini mustakbali ni wa matumaini.

 Pia Obama alizungumzia juu ya mgogoro wa kinyuklia  na Iran na kusema  Iran  yenye silaha ya nyuklia itashawishi mashindano ya silaha katika Mashariki ya kati na ni kitisho kwa usalama wa Israel.

No comments:

Post a Comment