Wednesday, September 26, 2012

Wapinzani wa serikali wapata mafanikio upande wa kaskazini ya Syria

Kwa  mujibu  wa  uchunguzi  wa  shirika  la  habari  la  AFP ,eneo  kubwa  la  kaskazini  mwa  Syria  karibu  na  mpaka na  Uturuki  haliko  tena  katika  udhibiti  wa  serikali  mjini Damascus.

 Kwa  mujibu  wa  jeshi  la  waasi  la  Syria  huru , FSA,  jeshi  hilo  linadhibiti  eneo  karibu  kilometa  100. Shirika  linaloangalia  haki  za  binadamu  nchini  Syria  lililo na  makao  yake  makuu  mjini  London , limesema  kuwa karibu  asilimia  80  ya miji  na  vijiji  katika  mpaka  na Uturuki  haiko  tena  katika  udhibiti  wa  serikali  kuu  mjini Damascus.


 Taarifa  za  wanaharakati  zinasema  kuwa katika  mapigano  makali  jana  watu  zaidi  ya  70 wameuwawa. Ndege  za  kivita  za  serikali zimeushambulia  mji  wa  Aleppo  na  jimbo  la  Homs  na Daraa  ambapo  watu  24  wameuwawa.

No comments:

Post a Comment