MSANII wa
kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul, anatarajia
kufanya usaili kwa ajili ya watu watakaotumika katika kurekodi video ya
wimbo wake mpya ambao utaachiwa hivi karibuni.
Mkurugenzi wa
kampuni ya One Touch Solutions, Petter Mwendapole alisema mjini Dar es Salaam
kuwa Diamond amefikia uamuzi huo katika kuhakikisha kazi zake zinafanyika katika
kiwango cha kimataifa.
“Jumamosi ijayo
tutafanya usaili wa watu ambao wataonekana kwenye video hiyo, hii ni mara ya
kwanza kwa kitu kama hiki kufanyika nchini kwetu ingawa wenzetu Ulaya wamekuwa
wanafanya hivyo na wanaonekana wanakuwa wanalipwa tofauti na video nyingi za
wasanii wa hapa kwetu na hao watakaochaguliwa kwenye video hiyo watalipwa pia,”
alisema.
Akizungumzia
kuhusu video hiyo, Mwendapole alisema itarekodi ndani na nje ya nchi ili
kuhakikisha inakidhi matakwa ya soko ambalo msanii huyo analiangalia kwa sasa
huku video hiyo ikifanya na kampuni bora kabisa Tanzania.
Kwa upande wake
Diamond alisema lengo kubwa la kufanya hivyo ni kuleta mapinduzi katika sekta ya
muziki nchini lakini pia kutengeneza ajira kwa ajili ya wasichana na wavulana
ambao wako mitaani lakini wanapenda muziki.
Diamond ambaye
alikuwa nchini Marekani wiki iliyopita anatarajiwa tena kwenda Marekani kwa
ajili ya onyesho moja la muziki.
Msanii huyo
alifanya mapinduzi katika medani ya muziki wa bongo baada ya kufanya onyesho
lake alilolipa jina la Diamond’s are Forever pale Mlimani City ambapo katika
shoo hiyo aliifanya mwenyewe na kiingilio kikiwa sh 50,000 jambo ambalo
halijawahi kufanyika katika ulimwengu wa muziki nchini.
thanks brother HAAZU /http://haazu.blogspot.com/ |
No comments:
Post a Comment