Maelfu kwa maelfu ya waislamu wameandamana katika kila pembe ya
ulimwengu wa kiarabu na Asia baada ya sala ya Ijumaa. Machafuko
yameripuka miongoni mwa kwengineko nchini Sudan ambako Ubalozi wa
Ujerumani umetiwa moto.
Mjini Khartoum wafuasi wasiopungua elfu tano wa itikadi kali ya dini ya
kiislamu wamezivamia ofisi za balozi za Uingereza na Ujerumani na
kuutia moto ubalozi wa Ujerumani. Kwa mujibu wa mashahidi na maripota wa
shirika la habari la Uingereza, Reuters, na lile la Ufaransa, AFP,
waandamanaji waliojaa hasira waliparamia jengo la ubalozi wa Ujerumani
na kupandisha bendera ya itikadi kali badala ya ile ya Ujerumani.
"Watumishi wa ubalozi wako salama" amesema waziri wa mambo ya nchi za
nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle, aliyewataka maafisa wa serikali ya
mjini Khartoum wachukue hatua zinazohitajika kudhamini usalama wa
wanadiplomasia. |
No comments:
Post a Comment