Marekani imesema hakuna taarifa zilizopatikana hadi
sasa zinazoonyesha kuwa mashambulizi
yaliyofanyika kwenye ubalozi wa nchini Hiyo mjini
Benghazi nchini Libya yalipangwa. Taarifa hiyo
inakuja wakati miili ya watu wanne waliouawa
kwenye mashambulizi dhidi ya ubalozi huo ikiwa
imeshawasili nchini Marekani.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jay Carne alisisitiza hapo kabla kwamba tukio la kushambuliwa kwa ubalozi huo bado linafanyiwa uchunguzi na kuwaambia waandishi wa habari kwamba hawana taarifa zinazoonyesha kuwa zilipangwa kabla.
Carney amesema ghasia zinazoonekana sasa kwenye nchi mbalimbali za ulimwengu wa kiarabu zinatokana na mkanda wa video ambao waislamu wengi wanauona kuwa umemdhalilisha mtume wa dini yao. Aidha amesema kuwa mashambulizi hayo si kumbukumbuku ya mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001 katika majengo pacha mjini New York kama inavyosemekana. Uongozi wa Libya na maafisa wa Marekani hapo kabla walisema kuwa mashambulizi hayo yalikuwa yamepangwa.

No comments:
Post a Comment