Saturday, September 15, 2012

Pope Benedict aanza ziara ya siku tatu Lebanon huko Beirut

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Benedict wa 16 ametoa wito wa kuwepo kwa amani katika ziara yake ya siku tatu nchini Lebanon. Papa Benedict amekutana na Rais wa nchi hiyo Michel Suleiman .

 Katika hotuba yake ya makaribisho, Papa alotolea mfano vuguvugu la mageuzi katika ulimwengu wa kiarabu akisema anatambua  mageuzi hayo yalivyofufua upya ''heshima ya waarabu''.


 Papa amesema utulivu miongo mwa dini mbalimbali nchini Lebnon unaonyesha mfano mzuri. Kiongozi huyo wa Kanisa katoliki pia ametoa wito wa kukomeshwa kwa vitendo vya uingizaji silaha kwenye eneo la mashariki ya kati ili kusitisha mzozo wa Syria.

No comments:

Post a Comment