Nchini Urusi, mmoja wa wapinzani
wakubwa wa rais Vladmir Putin na kiongozi wa maandamano ya hivi maajuzi
ya wafuasi wa upinzani, Gennady Gudkov, amefukuzwa bungeni.
Katika kura ya kwanza ya aina yake katika
kipindi cha miaka kumi na saba, wanasiasa wa bunge la waakilishi
linalofahamika kama DUMA, walionyesha kwa idadi kubwa kuunga mkono hatua
ya kutimuliwa kwa bwana Gudkov, kutokana na kile wanachozingatia kuwa
kujihusisha na biashara mbali mbali zinazohitalifiana na maadili.
Kutimuliwa kwake kuna maana kuwa amepoteza ulinzi wa sheria dhidi ya kushtakiwa.
Wafuasi wake wanasema hatua hiyo ilichochewa kisiasa.
No comments:
Post a Comment