Friday, September 14, 2012

Maandamano yasambaa katika ulimwengu wa Kiislamu




Ghasia katika maandamano ya kupinga filamu ya kumkashifu Mtume Muhammad mjini Cairo, Misri. Ghasia katika maandamano ya kupinga filamu ya kumkashifu Mtume Muhammad mjini Cairo, Misri.
Maandamano ya kupinga filamu hiyo sasa yanaendeela kuenea katika nchi nyingine za Kiislamu, ikiwemo Morocco, Sudan na Tunisia.

Mjini Tunis polisi nao wamelazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji.
Mjini Sanaa, Yemen, waandamanaji wenye hasira na filamu hiyo wamepambana vikali na polisi wakati wa maandamano yao nje ya ubalozi wa Marekani.


Filamu hiyo ambayo imesababisha machafuko na maandamano imeandaliwa na raia wa Marekani mwenye asili ya Kiyahudi ambaye anauelezea Uislamu kama kidonda ndugu na kumkashifu Mtume Muhammad .

Marekani yapeleka meli za kivita Libya

Wakati huo Marekani imetuma meli na manowari nchini Libya baada ya balozi wake kuuawa huku pia ikiamini kwamba shambulio hilo lilitekelezwa na al-Qaida na si raia wa kawaida.

Kiasi ya askari 50 wamepelekwa mjini Tripoli kwa ajili ya kuimarisha ulinzi katika ubalozi wake huku pia ikianza kuwaondoa wafanyakazi wake katika mji wa Benghazi.

Maandamano ya kulaani mauaji dhidi ya balozi wa Marekani nchini Libya. Maandamano ya kulaani mauaji dhidi ya balozi wa Marekani nchini Libya.
Rais Barack Oboma wa Marekani ameitaka Libya kuimarisha ulinzi lakini pia akitaka hatua zaidi kuchukuliwa kwa wote waliohusika na mauaji hayo.

Katika taarifa yake hapo jana waziri wa mamabo ya nje wa Marekani Hillary Clinton alisema mashambulizi hayo yalifanywa na kundi dogo na si raia wala serikali ya Libya.
Maafisa wa Marekani wanachunguza tukio hilo lakini wakiamini kwamba huo ulikuwa mpango wa Al qaeda ambao wametumia maandamano kulipiza kisasi wakati wa kumbukumbu ya septemba 11.
Marekani imeendelea kuwaonya raia wake katika mataifa kadhaa kuepuka kukaa katika umati mkubwa lakini inaimarisha ulinzi katika balozi zake zote.

Na Rais wa Afghanistan Hamid Karzai amelazimika kusitisha ziara yake nchini Norway akihofia ghasia zinazoweza kutokea kutokana na filamu hiyo.

No comments:

Post a Comment