Thursday, September 13, 2012

Obama alaani mauaji ya balozi wake Libya

Rais wa Marekani Barack Obama amelaani mashambulizi yaliyomuua balozi wa nchi yake nchini Libya jana. Obama alisema ameagiza kuchukuliwa kwa hatua zozote ili kuimarisha usalama wa maafisa wa Marekani nchini Libya, na balozi za nchi hiyo duniani kote.

Hata hivyo, Obama amesema mauaji hayo hayajateteresha uhusiano uliyopo baina ya Marekani na Libya. Mashambulizi hayo yametokea usiku wa kuamkia jana katika mji wa mashariki wa Benghazi kufuatia filamu iliyotengenezwa nchini Marekani, ikiukashifu Uislamu na Mtume Muhammad.


Balozi wa Marekani Christopher Stevens aliyekuwa Benghazi kwa ziara fupi aliuawa pamoja na maafisa wengine watatu wa ubalozi huo mdogo. Awali, waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton alisema waliyomuua balozi Stevens na maafisa wengine wanne siyo watu wa Libya wala serikali ya nchi hiyo, bali ni kundi dogo la kikatili.

No comments:

Post a Comment