Thursday, September 13, 2012

Rais mpya wa Somalia aponea chupuchupu

Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mahmoud amenusurika kuuawa leo, siku moja tu baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo.

 Mabomu mawili yalilipuka nje ya hoteli ambako Mahmoud na waziri wa mambo ya nje wa Kenya, Sam Ongeri, walikuwa wanafanya mkutano na waandishi wa habari, nje ya mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Gazeti la Kenya la Standars limeripoti kuwa viongozi hao wawili hawakupata madhara yoyote lakini miili miwili ilionekana katika mlango wa kuingilia hotelini hapo, mmojawapo ukidhaniwa kuwa ni wa mlipuaji wa kujitoa muhanga.


Taarifa zinasema wanajeshi watatu, mmoja kutoka Uganda, waliuawa katika mlipuko huo na kwamba walipuaji watatu nao waliuawa. Kundi la al-Shabaab limesema kwenye mtandao wake wa Twitter kuwa linahusika na mashambulizi hayo.  

No comments:

Post a Comment