Monday, September 17, 2012

Wafuasi wa Hezbollah kuandama leo Beirut



Wafuasi wa kundi la Hezbollah nchini Lebanon wanatarajiwa leo kuandamana kuipinga filamu inayomdhalilisha mtume Muhammad iliyotengenezwa nchini Marekani.

Maelfu ya wafuasi hao wanatarajiwa kushiriki maandamano hayo kufuatia mwito uliotolewa na kiongozi wa kundi hilo, Hassan Nasrallah, hapo jana. Maelfu ya watu waliandamana nchini Pakistan jana kuilaani filamu hiyo huku waandamanaji wakichoma bendera za Marekani na sanamu za rais wa Marekani, Barack Obama.



Waandamanaji hao walitaka Pakistan isitishe uhusiano na Marekani. Watu wasiopungua wanane walijeruhiwa wakati polisi walipokabiliana na waandamanaji katika ubalozi wa Marekani katika mji wa bandari wa Karachi. Balozi za kigeni katika mataifa ya kiislamu zimeendelea kuwa katika hali ya tahadhari kubwa huku Marekani ikihimiza kuwepo uangalifu.

No comments:

Post a Comment