Ujerumani imemkataza mchungaji mwenye msimamo mkali wa kidini
kutoka Marekani, Terry Jones, kuingia mjini Berlin kufuatua
maandamano katika nchi za kiislamu yaliyosababishwa na filamu
inayoudhalilisha Uislamu.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani iliyotolewa hapo jana. Akizungumzia mipango ya kundi lenye msimamo mkali kumualika mchungaji huyo kutoka Florida kuzuru Ujerumani, msemaji wa wizara hiyo amesema ziara ya Jones itakuwa kinyume na azma ya kudumisha amani ya umma. Jones, aliyesababisha maandamano makubwa kwa mipango yake ya kuichoma Quran hadharani, amesema filamu hiyo haikulenga kuwatusi Waislamu.
Inaripotiwa kwamba kundi hilo dogo linalojiita "Pro Deutschland" linataka kuandaa maonyesho ya filamu hiyo mjini Berlin. Kiongozi wa kundi hilo, Manfred Rouhs, ameliambia jarida la Der Spiegel la Ujerumani kuwa suala muhimu kwao ni uhuru wa kutoa maoni. Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani, Hans-Peter Friedrich, pia ameliambia jarida hilo kwamba atatumia kila njia ya kisheria kulizuia kundi hilo kuionyesha filamu hiyo.

No comments:
Post a Comment