Monday, September 17, 2012

Papa Benedict XVI arejea nyumbani

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani, Baba Mtakatifu Benedict XVI amerejea katika makao yake ya likizo huko Castel Gandolfo, yapata kilometa 30 kusini mwa mji mkuu wa Italia, Roma.

 Kiongozi huyo aliwasili jana usiku mjini humo baada ya kukamilisha ziara yake ya siku tatu nchini Lebanon ambako alitoa mwito kuwepo umoja kati ya Wakristo na Waislamu katika Mashariki ya Kati na amani katika nchi jirani ya Syria.


 Katika uwanja wa ndege wa mjini Beirut, Baba Mtakatifu alisindikizwa na rais wa Lebanon, Michel Suleiman, ambaye ni Mkristo na waziri mkuu wa nchi hiyo, Nagib Mikati, ambaye ni Muislamu wa madhehebu ya Sunni. Rais Suleiman alimshukuru papa Benedict XVI kwa ziara yake na kuahidi kuifanya Lebanon kuwa nchi ya mdahalo na uwazi.

No comments:

Post a Comment