Monday, September 17, 2012

Mazoezi ya kijeshi kufanywa Ghuba ya Uajemi

Meli za kivita kutoka nchi mbalimbali duniani zimekusanyika katika Ghuba ya Uajemi kwa kile ambacho jeshi la Marekani linakieleza kuwa ni mazoezi makubwa ya kijeshi ya kimataifa kuwahi kufanywa katika eneo la Mashariki ya Kati.

 Marekani inasema mazoezi hayo yaliyoanza jana yanajumisha mbinu za kuboresha kutambua na kuondoa mabomu ya kutegwa. Taarifa ya makao makuu ya jeshi la majini la Marekani imesema mazoezi hayo yatavishirikisha vyombo vya majini na maafisa kutoka nchi 30.


 Hata hivyo taarifa hiyo haikuzitaja nchi zinazoshiriki. Iran imetishia kutega mabomu katika mlango wa bahari wa Hormuz, ambapo asilimia 40 ya mafuta yanayouzwa katika nchi za nje, hupitia. Iran pia imetishia kuzishambulia kambi za jeshi la Marekani katika eneo hilo iwapo itashambuliwa.

No comments:

Post a Comment