Monday, September 17, 2012

Maandamano dhidi ya Japan yafanyika China

Maandamano ya kuipinga Japan yameendelea katika miji mbalimbali nchini China kuhusu visiwa vinavyogombaniwa katika bahari ya China Mashariki.

Polisi wa kupambana na fujo katika mji wa kusini wa Shenzhen walifyetua mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji. Katika mji ulio karibu wa Guangzhou, waandamanaji walizichoma bendera za Japan na kuivamia hoteli moja iliyo karibu na ubalozi wa nchi hiyo. Shirika la habari la serikali ya China limeripoti kwamba watu zaidi ya 10,000 walijitokeza kwenye maandamano hayo mjini humo.


 Waziri mkuu wa Japan, Yoshihiko Noda, ameitaka China kuhakikisha usalama wa Wajapan na biashara kufuatuia mashambulio ya Jumamosi iliyopita, dhidi ya Wajapan na magari yaliyotengenezwa nchini Japan. Waziri wa ulinzi wa Marekani, Leon Panetta, akiwa njiani kuelekea Tokyo Japan, ameonya kwamba China na mataifa mengine ya Asia huenda yakaingia vitani kuhusiana na mizozo ya mipaka kama serikali za nchi hizo zitaendelea na tabia ya uchochezi.

No comments:

Post a Comment