Monday, September 17, 2012

NATO yashambuliwa Afghanistan


Wapiganaji wa Taliban wameshambulia moja ya vituo muhimu cha vikosi vya kimataifa nchini Afghanistan, katika kambi ya Bastion iliyoko katika jimbo la Helmand.

Wanasema shambulio hilo ni kulipiza kisasi kupinga filamu inayoukashifu Uislamu iliyotengenezwa nchini Marekani, ambayo pia imesababisha maandamano ya ghasia katika nchi mbalimbali.
Katika shambulio hilo lililodumu kwa muda wa saa nne, Taliban walshambulia kambi hiyo ya Bastion kwa kutumia bunduki za rashasha, maguruneti, na maroketi.

Wanajeshi wawili wa Marekani waliuawa pamoja na wapiganaji wasiopungua kumi na watano wa Taliban.
Msemaji wa wanajeshi wa kimataifa nchini Afghanistan-ISAF, Luteni Kanali Hagen Messer amesema, ni mapema mno kusema iwapo shambulio hilo lina uhusiano wowote na filamu ya kimaraekani inayoshutumiwa kumkashifu mtume Mohammad.


Hata hivyo vikosi vya kimataifa nchini Afghanistan -ISAF vimekiri kuwa wapiganaji wa Taliban waliweza kushambulia kambi hiyo kutokana na mapungufu yake.

No comments:

Post a Comment