Mjumbe wa kimataifa kwa Syria, Lakhdar Brahimi, amesema mgogoro wa Syria unaelekea kubaya zaidi. Brahimi ameyasema hayo mjini Moscow hivi jana baada ya mazungumzo muhimu na waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov, kutafuta suluhisho la mzozo huo.
Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, ameelezea kufadhaishwa kwake na kushindwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kwa kipindi cha siku nne za Eid-el-Adh'ha.
"Sasa kila upande unaulaumu mwengine kwa kuvunja makubaliano haya ya kusitisha mapigano, Matokeo yake ni kwamba hakukuwa na kipindi cha mapumziko ya mapigano, na watu wa Syria hawakuitumia hata siku moja ya amani katika Iddi hii." Amesema Brahimi.
Urusi ilikuwa imeunga mkono mpango huo wa Brahimi na imeeleza kusikitishwa na kushindwa kwake. Hata hivyo, Lavrov amerejelea msimamo wa nchi yake kwamba, mzozo wa Syria utapatiwa suluhisho tu, pale mataifa ya Magharibi na majirani wa nchi hiyo, hasa Uturuki, watakapoanza kuzungumza moja kwa moja na Rais Bashar al-Assad, na sio upinzani tu.
No comments:
Post a Comment