Obama afuta kampeni zake kwa sababu ya Kimbunga Sandy
Rais Barack Obama wa Marekani amesitisha kampeni zake ili kujipa muda wa kushughulikia madhara ya Kimbunga Sandy kinachoikumba nchi hiyo kwa sasa.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu ya Marekani, Rais Obama hatokwenda tena Winsconsin hii leo ,alikuwa awe na mkutano wa kampeni, na badala yake atabakia Washington kufuatilia kimbunga hicho.
Tayari Rais Obama alishafuta mkutano wake wa kampeni katika jimbo la Florida uliokuwa ufanyike mchana wa jana .
Miji mikubwa ya pwani ya mashariki ya Marekani, kutoka New York hadi Washington, iko kwenye hali ya tahadhari ya kimbunga hicho kinachotembea kwa kasi ya kilomita 140 kwa saa. Tayari watu katika mji wa New Jersey wamehamishwa kuepuka madhara ya kimbunga hicho kinachotajwa na watabiri ya hali ya hewa kuwa kikubwa kabisa katika miaka ya karibuni.
No comments:
Post a Comment