Marekani yazinga msaada wa Algeria kuivamia kijeshi Mali
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton, yuko nchini Algeria, akitafuta msaada wa nchi hiyo kwa operesheni ya kijeshi nchini Mali.
Algeria, ambalo ni taifa lililo tulivu zaidi kaskazini mwa Afrika, inaonekana kama mchangiaji muhimu kwa upande wa intelijensia, ikiwa si kwa wanajeshi wa ardhini, kwa hatua yoyote ya kuwang'oa wanamgambo wa al-Qaida katika mpaka wake wa kusini.
Maafisa wa Marekani wamesema kwamba Bi Clinton amekutana na Rais Abdel-Aziz Bouteflika wa Algeria, na hoja ya Algeria kuonya dhidi ya uingiliaji kati kijeshi Mali ndiyo mada kuu ya mazungumzo yao.
Mpango huo wa kijeshi utaihusisha serikali ya Mali na majirani zake wa Afrika ya Magharibi wakiongoza kijeshi dhidi ya waasi wa kaskazini. Marekani na Umoja wa Ulaya zinauunga mkono mpango huo.
No comments:
Post a Comment