Tuesday, October 30, 2012

.Nyamwasa avuliwe ukimbizi



Generali Kayumba alikuwa mshirika wa karibu wa Rais Paul Kagame
Mashirika mawili ya kutetea haki za binadamu yameiomba mahakama moja ya Afrika Kusini kutoa amri ya kumvua hadhi ya ukimbizi aliyekuwa mkuu wa majeshi ya Rwanda Faustin Nyamwasa.
Mashirika hayo yanadai kuwa Uhispania na Ufaransa zina vibali vya kumchukua Generali Faustin Nyamwasa, na kumsafirisha katika nchi hizo kukabiliwa na sheria.
Aidha mashirika hayo yanasema kuwa Generali Nyamwasa anakabiliwa na tuhuma za kuhusika katika mauaji ya raia nchini Rwanda na Congo na kwa hivyo hafai kulindwa na sheria ya wakimbizi nchini Afrika Kusini.
Makundi hayo yanasema kuwa Jenerali huyo hafai kurudishwa nchini Rwanda, ambako anakabiliwa na hatari kwa maisha yake, lakini anafaa kushtakiwa nchini Ufaransa au Uhispania.

Serikali ya Rwanda ilidaiwa kutaka kumuua Nyamwasa mara mbili tangu alipowasili nchini Afrika Kusini mwaka 2010. Njama zote mbili zilitibuka.

No comments:

Post a Comment