Mwandishi wa habari wa Ugiriki akamatwa kwa kuchapisha orodha ya matajiri
Mwandishi wa habari mmoja wa Ugiriki amekamatwa kwa kuchapisha orodha ya Wagiriki wenye akaunti zao kwenye benki za Uswisi.
Costos Vaxevanis alitiwa nguvuni na polisi mjini Athens hapo jana akituhumiwa kuvunja sheria za faragha.
Orodha hiyo yenye majina zaidi ya 2000 ilikabidhiwa kwa mamlaka za Ugiriki mwaka 2010 na mkuu wa sasa wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Christine Lagarde, wakati huo akiwa waziri wa fedha wa Ufaransa.
Ugiriki inapambana na ukwepaji kodi na ufisadi, ingawa imeripotiwa kwamba hakuna uthibitisho wa waliomo kwenye orodha hiyo kuvunja sheria.
No comments:
Post a Comment