Kiongozi wa maandamano ya kumpinga rais wa Urusi Vladimir Putin amewekwa chini ya kifungo cha nyumbani juzi , baada ya kuhojiwa kuhusiana na madai kwamba alitaka kuhamasisha uasi wa umma.
Kamati ya uchunguzi ya Urusi ilisema Sergei Udaltsov mwenye umri wa miaka 35 ameamriwa kutoondoka kutoka makaazi yake, Kamati ya uchunguzi ambayo ndiyo chombo cha juu kabisa cha uchunguzi nchini Urusi, ilimpeleka Udaltsov katika ofisi zake kwa ajili ya mahojiano baada ya wachunguzi kuikagua nyumba yake kwa zaidi ya saa tano .
wakisindikizwa na maafisa wa kikosi maalumu waliofunika nyuso zao, na kuondoa mikoba kadhaa ya ushahidi. Uchunguzi huo ulifuatia kipindi kilichorushwa katika televisheni inayoiunga mkono serikali ya Urusi, kikionyesha kuwa Udaltsov alikuwa anapanga uasi dhidi ya serikali.
No comments:
Post a Comment