Maelfu ya wachimba migodi wa kampuni ya Gold Fields ya Afrika Kusini wametii amri ya muajiri wao iliyowataka kurudi kazini katika muda aliowapa, vinginevyo wapoteze ajira zao.
Karibu asilimia 80 ya wafanyakazi hao wapatao 15,000 waliokuwa katika mgomo haramu wameripoti kazini ili kuepuka kufukuzwa, Kampuni ya Gold Fields ambayo ni ya nne kwa uchimbaji wa dhahabu duniani ilitishia kuwafukuza kazi wafanyakazi hao kama wasingerudi kazini kufikia saa nane mchana.
Baada ya kutolewa kwa tangazo hilo, msemaji wa kampuni hiyo, Willie Jacobsz amesema wafanyakazi 8,000 kati ya 11,000 walioandikwa kufanya kazi katika mgodi wa magharibi wa KDC wa kampuni hiyo wameripoti kazini, lakini akaongeza kuwa kampuni hiyo ilitaka kuthibitisha kama walibaki kazini.
No comments:
Post a Comment