Mwanamume mwenye umri wa miaka 65 amefariki dunia kwa ugonjwa wa moyo wakati wa maandamano mjini Athens, Ugiriki ambapo polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kukabiliana na waandamanaji waliokuwa wakirusha mabomu ya petroli.
Afisa wa wizara ya afya nchini humo amesema mwanamume huyo alipelekwa hospitali ambako juhudi za kuokoa maisha yake zilishindwa, Vyanzo vya polisi vilisema mwanamume huyo aliokotwa katika benchi mbele ya kanisa, mita kadhaa kutoka sehemu ambako kulikuwepo na makabiliano na waandamanji.
wakati habari nyingine zikisema alikutwa katika uwanja wa Syntagma, karibu na eneo la tukio, Maelfu ya raia waliingia mitaani jana kushiriki maandamano mjini Athens na wengine waliandamana katika mji wa pili kwa ukubwa wa Thessolaniki kupinga hatua za kukaza mkaja zinazochukuliwa na serikali ya waziri mkuu Antonis Samaras kukabiliana na mgogoro wa madeni.
No comments:
Post a Comment