Ripoti ya Umoja wa mataifa inasema wafuasi wa aliyekuwa rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, wamekuwa wakijaribu kupata usaidizi kutoka kundi la wapiganaji wa Kiislamu kutoka Mali kwa ajili ya kampeni ya kuzusha ghasia nchini Ivory Coast.
Ripoti hiyo pia inawashutumu wafuasi wa Bwana Gbagbo kwa kujaribu kuchukua wanajeshi wa vikosi vya Mali kuwasaidia kunyakua madaraka kutoka kwa Rais wa sasa Bwana Alassane Ouattara.
Bwana Gbagbo anasubiri kesi yake katika mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai.
Wafuasi wa Bwana Gbabo wameielezea ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa kuwa ni uongo wa kimakusudi.
No comments:
Post a Comment