Ripoti ya Benki ya dunia kuhusu chakula barani Afrika inasema kuwa wakulima wanaweza tu kuzalisha chakula cha kutosha kulisha watu wa bara hilo ikiwa vikwazo vya biashara kati ya nchi hizo vitapunguzwa.
Mamilioni ya watu katika eneo la Sahel wanakumbwa na njaa na utapia mlo.
Kwa mujibu wa benki hiyo, tatizo la uhaba wa chakula litapunguka tu ikiwa wakulima katika maeneo yenye kuzalisha chakua wataweza kuruhusiwa kusafirisha mazoa yao kupitia mipaka bila malipo.
Kuondoa vikwazo vya mipakani, pia itapunguza gharama ya chakula.
Benki ya dunia inasema kuwa asilimia tano ya nafaka barani Afrika inatoka katika mataifa mengine ya Afrika ikisema kuwa mashamba makubwa yenye dhoruba hayatumiwi kwa upanzi.
No comments:
Post a Comment