Maelfu ya watu nchini Pakistan, wametia saini wito wa kutaka msichana aliyepigwa risasi na wapiganaji wa Taleban akitetea haki ya wasichana kusoma, atuzwe tuzo la amani la Nobel.
Watu wanataka Malala mwenye umri wa miaka 15, atuzwe kwa kuhatarisha maisha yake wakati akitetea haki za wasichana kila mahali.
Muigizaji mashuhuri, Angelina Jolie, ameunga mkono wito huo, ambao pia umeungwa mkono na wanasiasa nchini Canada.
Malala anapokea matibabu nchini Uingereza.
Babake amesema msichana huyo atarejea nchini Pakistan licha ya kutolewa vitisho vipya dhidi ya maisha yake.
No comments:
Post a Comment