Hofu leo imetanda karibu na ukanda wa Gaza baada ya shambulizi la angani la Israel kuwauwa wanamgambo wanne, nayo makundi yenye silaha ya Kipalestina yakavurumisha zaidi ya maroketi 70 kusini mwa Israel, na kuwajeruhi vibaya watu wawili.
Hilo ndilo ongezeko kubwa la ghasia za mipaka ya pande zote tangu mwezi juni, na kuilazimu Israel na makundi ya wanamgambo katika ukanda wa Gaza kuapa kuwa hawatakubali mashambulizi hayo kufanywa bila kujibiwa.
Mashambulizi hayo ya hivi punde yalianza jana jioni, muda mfupi baada ya kukamilika ziara ya ngazi ya juu katika ukanda wa Gaza na Mfalme wa Qatar, wakati wanamgambo walipofyatua maroketi sita kusini mwa Israel.
Israel kisha ikafanya mashambulizi mawili ya angani kaskazini mwa Gaza, na kuwauwa wanamgambo wawili kutoka kundi la Hamas, na kuwajeruhi watu wengine saba, na kuchochea mashambulizi mengine ya maroketi. Kufuatia machafuko hayo, Waziri wa Ulinzi wa Israel Ehud Barak amefutilia mbali mazungumzo na Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Mataifa aliyeko nchini humo Catherine Ashton, ili kuzuru eneo la mpakani la ukanda wa Gaza.
No comments:
Post a Comment