Sudan leo imeishutumu Israel kwa kukilipua kiwanda cha silaha na ikatishia kulipiza kisasi baada ya tukio hilo lililowauwa watu watatu.
Waziri wa Utamaduni na Habari wa Sudan Ahmed Bilal Osman amesema leo kuwa wanadhani Israel ndiyo iliyohusika na mlipuko huo, Amesema kuwa ndege nne zilihusika katika shambulizi hilo, lililotokea usiku katika kiwanda cha silaha cha Yarmouk Kusini mwa Khartoum.
Wakaazi wamesema ndege au kombora lilipiga juu ya kiwanda hicho muda mfupi kabla ya kulipuka na kuwaka moto.
Awali, Gavana wa jimbo la Khartoum Abdulrahman al Khider alisema uchunguzi wa mwanzo umebainisha kuwa mlipuko huo ulitokea katika ghala ya kuhifadhi silaha.
Alipuuzia mbali madai kwamba sababu nyingine zilisababisha tukio hilo, Khider amesema watu kadhaa wamelazwa hospitalini baada ya kupaliwa na moshi lakini hakuna aliyefariki.
No comments:
Post a Comment