Sherehe za leo zimekuwa za kipekee kwani ni sherehe za mwisho kuongozwa na Rais Kibaki huku Kenya ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu mwaka ujao chini ya katiba mpya na vilevile wakati ambao taifa hili litakuwa linatimiza miaka 50 tangu kupata uhuru mwaka ujao.
Kwenye hotuba yake ambayo imekuwa ya kutia moyo, Rais Mwai kibaki amezingatia hasa ufanisi ambao nchi hii imepiga miaka kumi tangu achukue hatamu za uongozi kutoka kwa mtangulizi wake Rais Mtsaafu Daniel Arap Moi mwaka 2002.
No comments:
Post a Comment