Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema wananchi wa taifa hilo wanahitaji kuzaliwa upya na kujifaharishia utaifa wao. Katika hotuba yake ya kwanza kwa taifa, tangu kurejea katika wadhifa wa urais, Rais Putin amesema nchi hiyo inakosa uungaji mkono wa dhati wa wananchi wake.
Mbele ya wageni waalikwa zaidi ya mia moja kwenye Ikulu ya Moscow, kiongozi huyo kuna haja ya kuweka msingi wa kuimarisha uungwaji mkono na jamii.
Vile vile, Putin amezungumzia madai mbali mbali ya mataifa ya magharibi dhidi ya nchi hiyo, akisema Urusi inafuata aina yake ya demokrasia na inapuuzia vigezo vyote vinavyotolewa na mataifa ya kigeni.
Wanasiasa ambao wanapata usaidizi kutoka nje, amesema hawana nafasi katika nchi hiyo. Rais Putin amezungumzia pia uundwaji wa nafasi milioni 25 za ajira, pamoja kutoa vivutio kwa madaktari na wahandisi. Jeshi la Urusi pia litaimarishwa.
No comments:
Post a Comment