Bomu la kutegwa ndani ya gari limeua watu wasiyopungua16, saba kati yao wakiwa watoto katika mji wa Qatana, kusini magharibi mwa Damascus, huku Urusi ikikiri kwa mara ya kwanza kuwa utawala wa rais Bashar al-Assad unaelekea kuanguka.
Shirika la uangalizi wa haki za binaadamu nchini Syria lenye makao yake mjini London, Uingereza, limesema bomu hilo lililoripukia nje ya makaazi ya wanajeshi na karibu na shule ya msingi, limeua watu 17, wakiwemo wanawake wawili na watoto saba.
Watu wengine 23 wamejeruhiwa katika mlipuko huo. Mji wa Qatana, ulioko kilomita 21 nje ya Damascus unakaliwa na wafanyakazi ambao wengi wao ni wasunni na wachache wakristu, na uko chini ya udhibiti wa jeshi.
Wakati huo huo, naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Mikhail Bogdanov ameliambia shirika la habari la Itar-Tass, kuwa utawala wa Assad unapoteza udhibiti wa nchi kwa kasi kubwa na kwamba hawaondowi uwezekano wa waasi kupata ushindi katika vita hivi.
No comments:
Post a Comment