Jambazi
sugu mkoani Arusha,Manyara na Kilimanjaro Ismail Nicolaus {46}
maarufu kwa jina la ‘’Tumbonii’’ limeuawa kwa kupigwa risasi na mtu
anayedaiwa kuwa ni jambazi mwenzake wakituhumiana kurushana fedha za
wizi.
Tukio
la kuuawa kwa jambazi hilo na mwenzake limetokea eneo la Bomangómbe
mkoani Kilimanjaro juni 22 mwaka huu na mwili wake kutelekezwa katika
hospital ya Mawenzi mkoni humo.
Habari za
uhakika ambazo zilisema kuwa Tumbonii aliuawa na jambazi
mwenzake kwa kupigwa risasi na
kufa hapo hapo katika tukio lililotokea eneo hilo.
Vyanzo vya
habari viliendelea kusema kuwa kupigwa risasi kwa tumbonii na huyo jambazi
mwenzake ni kufuatia kutapeliana mamilioni ya fedha walizoiba wiki moja kabla ya kifo chake.
Habari
zilisema kuwa jambazi aliyempiga risasi Tumbonii ndiye aliyekimbia na mamilioni
hayo ya fedha.
‘’Wale
majambazi walitapeliana na marehemu alitangaza kumuua pindi
watakapokutana lakini amekufa yeye baada ya mwenzake kumwai''alisema
mtoa
habari
Habari zilisema marehemu Tumboni
aliokotwa na kupelekwa katika chumba cha maiti cha hospital ya mkoa ya Mawenzi
mkoani Kilimanjaro .
Vyanzo hivyo
vilisema ndugu marehemu alipopata taarifa za nduguye kuuawa
alikwenda polisi Arusha ili kupata taarifa lakini alidai
kuwa hakupata ushirikiano juu ya hilo lakini polisi wema walimwambia kuwa
nduguye yuko chumba cha maiti Moshi na ameuawa.
Habari
zilisema alikwenda Hospital ya Mawenzi juni 26 mwaka
huu na kuuchukua mwili huo leo Jambazi Tumbonii amezikwa nyumbani kwake
Kimandolu Jijini Arusha.
Kamanda wa
polisi Mkoani Arusha Liberatus Sabas alipoulizwa juu ya kifo cha jambazi huyo
alisema kuwa hana taarifa juu ya hilo lakini alikiri kuwa jambazi huyo alikuwa
akitafutwa sana na jeshi hilo kwa muda mrefu bila ya mafanikio kutokana
kutokana na kuhusika na uhalifu mkoani
No comments:
Post a Comment