Mahakama Ubelgji yarusu uchunguzi kifo cha Lumumba
Mahakama ya rufaa ya mjini Brussels, imeamua jana Jumatano kuwa waendesha mashitaka wa Ubelgiji wanaweza kuanzisha uchunguzi juu ya mauaji ya waziri mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Patrice Lumumba yaliyotokea mwaka 1961.
Mahakama hiyo ya rufaa imesema mauaji hayo huenda yakawa ni uhalifu wa kivit, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, ambayo zamani ilikuwa inajulikana kama Zaire, ilipata Uhuru wake kutoka kwa Ubelgji mwaka 1960.
Kesi hiyo ilifunguliwa mwaka 2010 na mmoja wa watoto wa Lumumba, akiwashtaki raia kadhaa wa Ubelgji, ambao aliwatuhumu kushiriki katika mauaji ya baba yake, Wanane kati ya watuhumiwa hao bado wako hai, Wakati wa kifo cha Lumumba, washirika wa nchi za magharibi walimshtumu kwa kutaka kuiunganisha nchi yake na Muungano wa Kisovieti.
Alipinduliwa wiki chache tu baada ya Kongo kupata uhuru wake. Bunge la Ubelgiji liligundua hapo awali kuwa Lumumba alipelekwa kusini mwa mkoa wa Katanga, alikoteswa kabla ya kupigwa risasi na wanajeshi waliokuwa wanatekeleza maagizo ya maafisa wa Ubelgji.
No comments:
Post a Comment