Afisa Polisi wa Ujerumani atiwa hatiani kwa kifo cha mkimbizi
Mahakama ya mjini Magdeburg nchini Ujerumani imemtia hatiani kwa kosa la kuuwa bila kukusudia, Afisa mmoja wa Polisi kuhusiana na kifo cha raia wa Sierra Leone aliyekuwa anaomba hifadhi nchini Ujerumani, Oury Jalloh.
Mahakama hiyo pia imemuamrisha afisa huyo, kulipa faini ya euro 10.800. Oury Jalloh alifariki tarehe 7 Januari 2005 akiwa katika kizuizi cha polisi, Alidaiwa kuchoma godoro lake kwa moto hali ya kuwa mikono yake na miguu vilikuwa vimefungwa,Kwa hukumu hiyo, mahakama imezidisha ombi la wakili wa mashtaka aliyetaka mshtakiwa aliyetajwa kwa jina la Andreas S,aliekiri makosa, kulipa fidia ya euro 6,300.
Majaji wamesema katika hukumu hiyo kuwa kitengo kilichokuwa kinaongozwa na Andreas kilishindwa kufika kwa wakati kunusuru maisha ya Jalloh hata baada ya kulia kwa king'ora cha kuashiria kuna moto. Katika hukumu ya kwanza mwaka 2008, Andreas aliachiwa huru kutokana na makosa katika mashtaka, lakini kesi hiyo ilifunguliwa upya.
No comments:
Post a Comment