Waziri wa mambo ya kigeni wa Israel, Avigodor Lieberman, amesema leo kuwa anajiuzulu baada ya kushtakiwa kwa makosa ya udanganyifu na kuvunja uaminifu.
Hatua ya kujiuzulu kwa Lieberman inaweza kuwa na athari katika uchaguzi mkuu ujao nchini Israel. Katika taarifa aliyoitoa kwa njia ya barua pepe, Lieberman amesema anajua alitenda makosa na hivyo ameamua kujiuzulu nafasi yake ya waziri wa mambo ya kigeni na naibu waziri mkuu, na kuongeza kuwa ana matumaini atasafisha jina lake pasipo kuchelewa.
Kura za maoni zimenonyesha kuwa chama cha mrengo wa kulia cha Lieberman na waziri mkuu Benjamni Netanyahu kinaweza kushinda uchaguzi wa januari 22, lakini haijabainikwa wazi kama kuondoka kwakwe kunaweza kuathiri matokeo.
No comments:
Post a Comment