Kampeni za mwisho mwisho zinaendelea nchini Misri, ambapo makundi hasimu yanajaribu kuwashawishi wapiga kura wapatao milioni 51 kushiriki kura ya maoni juu ya rasimu ya katiba mpya hapo kesho na Jumamosi itakayofuata Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa mbili asubuhi hadi saa moja jioni katika miji ya Cairo, Alexandria, na majimbo mengine manane, na maeneo mengine yatapiga kura Jumamosi ya tarehe 22. Jeshi la Misri limepewa mamlaka ya polisi kwa muda kusaidia kuhakikisha usalama hadi matokeo ya mwisho yatakapotangazwa, Jumla ya wanajeshi 120,000 watasaidiana na polisi 130,000 wakati wa zoezi hilo. Kambi ya rais Muhammad Mursi inasema katiba hii inahitajika kukamilisha mchakato wa kuelekea demokrasia, baada ya miongo mitatu ya utawala wa Hosni Mubarak. Wapinzani wanasema katiba hiyo imeandaliwa vibaya na imeharakishwa bila kuwepo na muafaka.
No comments:
Post a Comment