Urusi imepuuza kauli iliyotolewa na mwanadiplomasia wa ngazi ya juu nchini humo, kuwa rais Bashar al-Assad anaweza kushindwa katika vita dhidi ya waasi, huku mataifa ya magharibi yakizidisha shinikizo kwa utawala wake, na bunge la Ujerumani likiidhinisha uwekaji wa mitambo ya kuzuia makombora nchini Uturuki. Naibu waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi, Mikhail Bogdanov, alinukuliwa hapo awali akisema Assad alikuwa anapoteza udhibiti kwa kasi kubwa na kwamba waasi wanaweza kumuangusha wakati wowote. Lakini wizara ya mambo ya kigeni ya Urusi imesema waziri Bogdavo alirejerelea tu msimamo wa nchi hiyo kuhusu Syria.
No comments:
Post a Comment