Chama cha Hamas kimefanya mkutano wake wa kwanza katika Ukingo wa Magharibi jana, baada ya kupigwa marufuku kwa kipindi cha miaka mitano. Mkutano huo ulikuwa unasherehekea miaka 25 ya kuanzishwa kwa chama hicho cha Kiislamu. Maelfu ya Wapalestina walihudhuria mkutano huo uliyofanyika katika mji wa Nablus, huku wakipeperusha bendera za kijani za Hamas. Mkutano ulifanyika baada ya mamlaka ya Palestina kuondoa marufuku dhidi ya mikutano ya Hamas, iliyowekwa mwaka 2007, pale wapiganaji wa Hamas walipochukua udhibiti wa ukanda wa Gaza, baada ya vita vifupi na Fatah. Vyama hivyo vilianzisha mazunguzo ya maridhiano mwaka uliopita lakini hakukuwa na matokeo ya kuridhisha, lakini totauti zao zilipungua kufuatia uvamizi wa Israel dhidi ya Gaza mwezi uliopita wa Novemba. Kufuatia ruhusa ya kufanya mikutano yake mjini Nablus na Hebron leo, Hamas nayo imekubali kuruhusu mikutano ya Fatah mjini Gaza siku ya mwaka mpya.
No comments:
Post a Comment