Waripuaji wa kujitoa mhanga wamefanya mashambulizi kwenye kituo cha polisi nchini Pakistan na kuwaua watu sita, wakiwemo wanawake watatu. Mashambulizi hayo yalitokea katika mji wa Bannu, karibu na jimbo la Waziristan ya kaskazini, ambalo lina kiasi fulani cha kujiamlia mambo yake, na ambalo ni ngome ya wanamgambo wa kiislamu. Jimbo hilo pia liko mpakani na Afghanistan, na Marekani imekuwa ikisema kuwa linatumiwa katika matayarisho ya mashambulizi nchini Afghanistan.
No comments:
Post a Comment