Wednesday, January 23, 2013

Clinton atoa ushahidi bungeni

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton, ametetea hatua zilizochukuliwa kuhusiana na mashambulio yaliyofanywa kwenye  ubalozi mdogo wa Marekani katika mji wa Benghazi nchini Libya. Mashambulio hayo yalitishia kulichafua jina la waziri huyo.
 Akizungumza bungeni kutoa ushahidi waziri Clinton alisema anachukua dhamana ya yaliyotokea kwenye ubalozi huo. Clinton ametoa ushahidi baada ya kuahirishwa kwa muda wa zaidi ya  mwezi mmoja kutokana na kuwa na afya mbaya. Ameonya juu ya changamoto zinazoweza kusababishwa na uasi unaozidi nguvu baada ya vuguvugu katika nchi za kiarabu.
Clinton amejitetea kwamba shambulio hilo la Beghazi halikutokea kufuatia pengo la kiusalama katika ubalozi wake mdogo na kwamba anawahurumia wote waliopoteza wapendwa wao katika tukio hilo.  Amewatolea mwito  wabunge wa Marekani kutokubali kuyaachia mwanya makundi ya wenye itikadi kali kukita mizizi katika nchi za kiarabu kwa kuwa hilo litachangia kuutishia usalama wa Marekani.

No comments:

Post a Comment